Kutoka hakielimu
1. Tunafurahi kwamba kiwango cha bajeti ya sekta nzima kimeendelea kuongezeka kutoka Trilioni 3.46 2014/15 hadi trilioni 3.88. Hata hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa ongezeko hili ambalo ni sawa na takribani asilimia 10 tu ya fedha iliyopangwa mwaka jana, si ongezeko linaloweza kuleta mabadiliko yanayoonekana katika sekta ya elimu hasa ukizingatia kuwa thamani ya shilingi imeshuka na mfumuko wa bei umeongezeka. Inawezekana ongezeko hili ni matokeo ya urekebishajiwa mfumuko wa bei badala ya ongezeko halisi katika matumizi.
2. Hata hivyo uchambuzi unaonesha kuwa bado kiwango cha fedha za bajeti ya sekta kinachopangwa ni asilimia kati ya 15 – 17 ya bajeti nzima ya serikali. Wakati tunaamini kuwa kiwango cha asilimia 17 si kibaya, lakini ni muhimu kujua kuwa bado ni kidogo ukilinganisha na majirani zetu Kenya, Rwanda, na Uganda ambao wamefikia walau asilimia 20 -25. Na zaidi Tanzania hatujaweza hata kufikia kiwango kilichokubaliwa cha huko Darkar Senegal chini ya EFA, cha kuwekeza hadi walau asilimia 20 ya bajeti ya taifa katika elimu.
3. Lakini pia tunafurahi kuwa sekta ya elimu imeendelea kupewa kipaumbele kwa maana ya kuwa sekta inayopokea kiasi kikubwa zaidi cha bajeti ya serikali. Wakati ikipangiwa trilioni 3.46 mwaka jana sekta ya miundombinu ambayo ilifuatia ilipokea takribani trilioni 2.3 wakati mwaka huu sekta ya elimu imepangiwa trillion 3.88 wizara inayofuatia ambayo ni miundombinu imeshuka zaidi hadi takribani Trilion 1.9.
4. Hata hivyo bado kuna mapungufu makubwa ambayo kama shirika tungependa yafanyiwe kazi;
Kiwango cha fedha zinazokwenda kwenye matumizi ya kawaida bado ni kikubwa sana kuliko kinachokwenda kwenye matumizi ya maendeleo ambayo ni muhimu zaidi. Mathalani katika makadirio ya Trilioni 3.88 yanayopendekezwa mwaka huu wa fedha, 84% zimeelekezwa katika matumizi ya kawaida huku asilimia 16 pekee (bilioni 604) ndizo zinaombwa kwaajili ya maendeleo.
Lakini bado hata hicho kiwango cha asilimia 16 za maendeleo hakipelekwi Wizara ya TAMISEMI ambayo inahusika na kutekeleza miradi ya maendeleo Elimumsingi kwa maana ya msingi, sekondari na vyuo. Mchanganuo unaonesha ni asilimia 20 tu ya fedha ya maendeleo inapelekwa TAMISEMI na 80 iliyobaki inapelekwa Wizara ya Elimu ambao ni watengenezaji wa sera na usimamizi wake na sio watekelezaji wa miradi.
Hata hivyo kinachofanywa na serikali hapa, ni kuhamishia fedha nyingi za maendeleo kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu. Mathalani takribani asilimia 91 ya bajeti nzima ya maendeleo ya Wizara ya Elimu, imeelekezwa kwa Elimu ya juu, hii ikimaanisha fedha nyingi pia za maendeleo zitaenda kugharamia mikopo ya wanafunzi elimu ya juu badala ya miradi ya maendeleo. Uzoefu wa mwaka uliopita unaonesha zaidi ya asilimia 67% ya bajeti ya maendeleo ya wizara ilikwenda kwa Bodi ya Mikopo na 33% tu ndiyo ikaenda kwa miradi ya maendeleo.
HakiElimu tumeona pia bajeti ya sekta ya elimu ikisambazwa katika wizara zaidi ya tatu kwa ajili ya utekelezaji. Madhara ya utaratibu huu ni kuwa fedha nyingi zinaelekezwa katika kugharamia idara na watumishi wa idara badala ya kuelekezwa moja kwa moja katika uwekezaji. Lakini pia kunakuwa hakuna uwazi na ni vigumu kwa bajeti hii kufuatiliwa utekelezaji wake. Na hii inaweza kuwa mwanya wa rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma.
Changamoto nyingine ambayo imekuwapo na imeendelea kujitokeza katika bajeti ya mwaka huu, ni utegemezi wa bajeti ya maendeleo kwa wahisani. Uchambuzi unaonesha bado takribani aslimia 50% ya bajeti ya maendeleo sekta ya elimu inatarajiwa kutoka kwa wahisani.
Athari za kutegemea wahisani zinafahamika, ahadi zao zimekuwa hazitimizwi; fedha imeendelea kuchelewa kutolewa na hivyo kurudisha nyuma utekelezaji wa miradi, mathalani utoaji wa ruzuku na kutokamilika kwa miradi mingine ya uwekezaji. Tunadhani ni muhimu serikali kuangalia uwezekano wa kutumia fedha za ndani kufadhili bajeti ya maendeleo.
5. Changamoto nyingine, ni kutokuwepo kwa uwiano kati ya bajeti inayopangwa, fedha ambazo hutolewa na Hazina au wahisani na kiwango ambacho hasa kinatumika katika utekelezaji wa mipango na bajeti. Kwa miaka mingi wizara, halmashauri na taasisi zimekuwa zikitekeleza bajeti pungufu kutokana na kutopatiwa kiwango sahihi kilichopangwa katika bajeti, na hata kinachotolewa hakitolewi kwa wakati.
Mathalani katika mwaka wa fedha 2011/12 kiasi cha shilingi bilioni 129.6 zilipangwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ya wizara ya elimu lakini ni shilingi bilioni 88.03 tu zilizotumika kutokana na nakisi ya bajeti. Aidha mwaka 2012/13 kiasi cha shilingi bilioni 140 kilipangwa kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya wizara lakini ni shilingi bilioni 78 tu sawa na asilimia 56 tu ndicho kilichotumika. Aidha mwaka 2014/15 shilingi bilioni 453.6 ziliidhinishwa lakini ni shilingi bilioni 335 ndizo zilizotumika sawa na asilimia 73.
Nakisi katika bajeti pia inaathili utekelezaji wa miradi na program kama vile upelekeaji wa ruzuku shuleni, mfano katika mwaka wa fedha 2013/14 wastani wa shillingi 4200 tu badala ya shilingi 10,000 kwa kila mwananfunzi zilipelekwa shule za msingi wakati wastani wa shilingi 12,000 tu ukifika shule za sekondari badalaya shilingi 25,000 kwa kila mwanafunzi. Aidha katika mwaka wa fedha 2014/15 hadi kufikia mwezi Mei 2015 serikali ilikuwa imepeleka shuleni wastani wa shilingi 1812 badala ya 10,000 kwa shule za msingi na wastani wa shilingi 5800 tu badala ya 25, kwa shule za sekondari.
Hivyo wakati mijadala ikiendelea juu ya elimu ni muhimu serikali ifikirie upya suala hili la uwiano kati ya fedha inayoidhinishwa, iliyotolewa na kiasi halisi kilichotumika.