Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

Kiwango cha ufaulu mitihani kupandishwa

Dk. Shukuru Kawambwa

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imezindua mpango wa utekelezaji wa mikakati ya matokeo makubwa sasa, unaolenga kupandisha kiwango cha ufaulu kwenye matokeo ya mtihani wa shule za msingi kwa darasa la saba, hadi kufikia asilimia 60 kwa mwaka huu, toka kiwango cha asilimia 31 cha mwaka jana.

Aidha, mkakati huo unalenga pia kupandisha kiwango cha ufaulu kwenye matokeo ya kidato cha nne toka asilimia 43 cha mwaka jana, hadi asilimia 60 kwa mwaka huu.


Akizindua mpango huo jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema uzinduzi uliofanyika ni matokeo ya mkutano wa washiriki 34 kutoka taasisi 31 zikiwamo za serikali na zisizo za serikali, washirika na wadau wa maendeleo ya elimu, waliokutana mwaka huu, kwa wiki sita na kutafakari kwa kina changamoto zinazoathiri sekta ya elimu.


“Walikutana hapa Dar es Salaam na changamoto kubwa walioanisha ni utambuzi kuwa, ingawa kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi kimeongezeka, lakini ubora wa elimu umeshuka, hususani kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu katika elimu ya msingi na sekondari,” alisema.


Alisema, ili kurekebisha hali hiyo, maabara iliangalia kwa makini namna ya kutatua baadhi ya changamoto na kuamua maeneo yatakayolengwa yenye matokeo makubwa muhimu na ambayo yanahitaji muda mfupi kutekelezwa, na hivyo kuweka mikakati tisa ya kutekeleza.


Mojawapo ya mikakati hiyo ni upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba, wanafunzi wanamudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu wakiwa darasa la pili, kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata.


Mikakati mingine ni upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza hadi ya mwisho,utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri, kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule na utoaji wa mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK.

 

CHANZO: NIPASHE

Share