Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Mr. Abdulmalik S. Mollel.
Katika mkutano wake na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Education Link ambao ni mawakala wa vyuo vya nje ya nchi. Alisema, "Tumeamua kuunga mkono serikali kwa mkono wa pili kwani wao wameonyesha njia kwa vyuo vya ndani ya nchi na sisi kama GEL tutakopesha wanaosoma nje ya nchi katika fani mbalimbali."
Katika mkutano wake na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Education Link ambao ni mawakala wa vyuo vya nje ya nchi. Alisema, "Tumeamua kuunga mkono serikali kwa mkono wa pili kwani wao wameonyesha njia kwa vyuo vya ndani ya nchi na sisi kama GEL tutakopesha wanaosoma nje ya nchi katika fani mbalimbali."
Pia Mr. Mollel alizungumzia kuhusu taasisi ya Global iliyojikita
katika tasnia hiyo kwa takribani miaka 7 sasa na kuongeza kuwa wamefikiria
kuanza kuwakopesha wanafunzi ili kuweza
kuinua maendeleo ya elimu nchini ambao utaenda sambamba na mpango wa sekta ya
elimu wa matokeo makubwa (Big results) .
(Bw
Abraham A. kiishweko meneja
masoko wa GEL kanda ya kaskazini
akifafanua jambo kwa wanafuzi wa shule
ya secondari ILboru kuhusu utaratibu wa
kusoma nje ya nchi)
Wazazi wengi wamekuwa wanakosa fursa ya kupeleka watoto wao
nje ya nchi kwa kukosa pesa ya mkupuo ya kuwalipia watoto wao kutokana na majukumu
mbalimbali, hii ikiwa changamoto kubwa kwa GEL ndio imepelekea kuanzisha programu
hii kwa kushirikiana na Bank of Africa (BOA).
Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Mr Abdulmalik (Katikati mwenye tai) akiwa katika mojawapo ya vyuo vya nje ya nchi na wanafunzi waliopitia GEL.
Kupitia fursa hiyo wanafunzi wataweza kukopeshwa bila riba na faida nyingine kadha
wa kadha ambazo alisema zitafafanuliwa siku ya jumapili tarehe 3 Novemba 2013 Serena Hotel, ambapo watakuwa
wakizindua mpango huo.
Pamoja na kufaidika na mkopo pia wanafunzi watafaidika na
masuala ya kupata udahili wa moja kwa moja kushughulikiwa suala la Visa na
kusindikizwa mpaka chuoni ambapo kuna mfumo wa uangalizi upande wa matokeo na
maudhurio aliongeza mkurugenzi mtendaji wa GEL.
Katika kujibu baadhi ya maswali ya wandishi wa Habari alisema
wanafunzi watakuwa wakiomba kupitia online na kwa mfumo wa central admission system ambao tayari
marekebisho yake yameshakamilika ,na kuhusu vyuo kuna baadhi vitakavyopewa kipaumbele
kwa nchi za Ukraini,India, china, Canada, U.S.A ,Malaysia na Uingereza na
mikopo hiyo itakuwa kwa ngazi za diploma mbaka shahada ya uzamili.
Katika kutimisha suala hilo Mr Mollel alisisitiza siku ya
uzinduzi wa programu hiyo ambayo ni jumapili ya Tarehe 3 novemba 2013 katika
ukumbi wa hotel ya serena.