Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles
Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2013,
kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis
Felix
Ufaulu kwa madaraja
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza
matokeo ya kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la
shule 20 za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za
Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu
Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611
walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85,
wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.
Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema.
Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa kujitegemea
Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.
Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa
na mwaka 2012 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na
asilimia 64.96 ya wote waliofanya mitihani hiyo.
Ufaulu kwa madaraja
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa
na asilimia 0.76 ya wote waliofanya mtihani huo walipata daraja la
kwanza, kati yao wavulana wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na
wasichana 137 sawa na asilimia 0.99.
Shule za Zanzibar zaboronga
Shule zilizofanya vizuri zenye watahiniwa chini ya 30,
Shule zilizofanya vizuri
Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa zaidi ya 30,
Waliopata daraja la pili ni 5,372 sawa na asilimia 12.54
wavulana wakiwa ni 3,142 sawa na asilimia 10.84 na wasichana 2,230 sawa
na asilimia 16.08.
Waliopata daraja la tatu ni 30,183 sawa na asilimia 70.45 wavulana wakiwa ni 20,442 sawa na asilimia 70.55 na wasichana 9,741 sawa na asilimia 70.24.
Waliopata daraja la tatu ni 30,183 sawa na asilimia 70.45 wavulana wakiwa ni 20,442 sawa na asilimia 70.55 na wasichana 9,741 sawa na asilimia 70.24.
Watahiniwa waliopata daraja la nne 4,362 sawa na
asilimia 10.18 ya wote waliofanya mtihani huo huku wavulana wakiwa ni
3,184 sawa na asilimia 10.99 na wasichana 1,178 sawa na asilimia 8.49.
Waliofeli ni 2,604 sawa na asilimia 6.08 wavulana wakiwa 2,021 sawa na asilimia 6.97 na wasichana 583 sawa na asilimia 4.20.
Shule za Zanzibar zaboronga
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, shule kutoka
Zanzibar zimefanya vibaya ambapo katika kundi la shule 10 za mwisho
zenye watahiniwa zaidi ya 30, saba zinatoka kwenye visiwa hivyo.
Kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 30,
nne zinatoka Unguja huku shule nyingine kongwe zilizokuwa zikifanya
vizuri mwaka huu zimevuta mkia.
Kwa upande wa shule 10 za mwisho zenye watahiniwa
zaidi ya 30 ya kwanza kutoka mwisho ni
Pemba Islamic College (Pemba),
Mazizini (Unguja),
Bariadi (Simiyu),
Hamamni (Unguja),
Dunga (Unguja),
Lumumba (Unguja),
Osward Mang’ombe (Mara),
Green Acres (Dar es Salaam),
High View International (Unguja)
na Mwanakwerekwe (Unguja).
Shule zilizofanya vizuri zenye watahiniwa chini ya 30,
ya kwanza kutoka mwisho ni
Mbarali Preparatory (Unguja),
Philter
Federal (Unguja),
St Mary’s (Dar es Salaam,
Mzizima (Dar es Salaam),
Hijra Seminary (Dodoma),
Tweyambe (Kagera),
Mpapa (Unguja),
Al-Falaah
Muslim (Unguja),
Presbyterian Seminary (Morogoro)
na Nianjema
(Morogoro).
Shule zilizofanya vizuri
Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa chini
ya 30,
ya kwanza ni
ya kwanza ni
Palloti Girls (Singida),
St. James Seminary,
Parane
na Sangiti (zote Kilimanjaro),
Itamba (Njombe),
Masama (Kilimanjaro),
Kibara (Mara),
St.Luise Mbinga Girls (Ruvuma),
St. Peters Seminary
(Morogoro)
na Peramiho Girls (Ruvuma).
Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa zaidi ya 30,
ya Kwanza ni
Mariani Girls (Pwani),
Mzumbe (Morogoro),
Feza Boys
(Dar es Salaam),
Iliboru na Kisimiri (zote kutoka Arusha),
St Mary’s
Mazinde juu (Tanga),
Tabora Girls (Tabora),
Igowole (Iringa),
Kibaha
(Pwani)
na Kifungilo Girls (Tanga).
Waliofaulu Sayansi
Waliofaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi na michepuo yao
kwenye mabano ni
Erasmi Inyanse kutoka Iliboru (PCM),
Maige Majuto
kutoka Kisimiri Arusha (PCM),
Gasper Mung’ong’o kutoka Feza boys Dar es
Salaam (PCM),
Gasper Setus kutoka St. James Seminary Kilimanjaro (PCM)
na msichana pekee kwenye kundi hili aliyeshika nafasi ya tano ni
Lucylight Mallya kutoka Marian Gils Pwani (PCM).
Waliofaulu Biashara
Kundi hili linaongozwa na
Eric Robert Mulugo
Tusiime Dar es Salaam (ECA),
Alicia Filbert kutoka Shule ya Ngaza Mwanza
(ECA),
Evart Edward, Kibaha Pwani (ECA),
Annastazia Renatus Tambaza Dar
es Salaam (ECA),
Peterson Meena Mbezi Beach Dar es Salaam (ECA).
Lugha na Sayansi ya Jamii
Wa kwanza ni
Asia Idd Mti kutoka shule ya
Barbro-Johansson ya Dar es Salaam (HGE),
Godlove Geofrey Ngowo kutoka
shule ya Majengo Kilimanjaro (EGM),
Jonson Elimbizi Macha kutoka shule
ya Njombe iliyopo Njombe (EGM),
Hamisi Joseph Mwita Iliboru Arusha (HGL)
na Sia Sand Marian Girls Pwani (EGM).
Matokeo yaliyozuiliwa na kufutwa
Dk Msonde alisema kuwa, Necta imezuia matokeo ya
watahiniwa 116 kutoka na sababu mbalimbali, 93 hawakulipa ada ya
mtihani, 10 walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya
mitihani na 17 walipata matatizo ya kiafya na hawakufanya mtihani hata
mmoja.
Alisema pia kuwa, baraza hilo limefuta matokeo ya
watahiniwa wanne kutokana na kubainika kufanya udanganyifu, kati yao
mmoja akiwa ni mtahiniwa wa shule na watatu wa kujitegemea.