Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WANAOSOMA NJE YA NCHI KUKOPESHWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Mr. Abdulmalik S. Mollel.

Katika mkutano wake na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Education Link ambao ni mawakala wa vyuo vya nje ya nchi. Alisema, "Tumeamua kuunga mkono serikali kwa mkono wa pili kwani wao wameonyesha njia kwa vyuo vya ndani ya nchi na sisi kama GEL tutakopesha wanaosoma nje ya nchi katika fani mbalimbali."


Pia Mr. Mollel alizungumzia kuhusu taasisi ya Global iliyojikita katika tasnia hiyo kwa takribani miaka 7 sasa na kuongeza kuwa wamefikiria kuanza kuwakopesha wanafunzi  ili kuweza kuinua maendeleo ya elimu nchini ambao utaenda sambamba na mpango wa sekta ya elimu wa matokeo makubwa (Big results) .


 (Bw  Abraham A. kiishweko  meneja masoko wa  GEL kanda ya kaskazini akifafanua jambo kwa  wanafuzi wa shule ya secondari  ILboru kuhusu utaratibu wa kusoma nje ya nchi)

Wazazi wengi wamekuwa wanakosa fursa ya kupeleka watoto wao nje ya nchi kwa kukosa pesa ya mkupuo ya kuwalipia watoto wao kutokana na majukumu mbalimbali, hii ikiwa changamoto kubwa kwa GEL ndio imepelekea kuanzisha programu hii kwa kushirikiana na Bank of Africa (BOA).



 Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Mr Abdulmalik (Katikati mwenye tai) akiwa katika mojawapo ya vyuo vya nje ya nchi na wanafunzi waliopitia GEL.

Kupitia fursa hiyo wanafunzi wataweza  kukopeshwa bila riba na faida nyingine kadha wa kadha ambazo alisema zitafafanuliwa siku ya jumapili  tarehe 3 Novemba 2013 Serena Hotel, ambapo watakuwa wakizindua mpango huo.


Pamoja na kufaidika na mkopo pia wanafunzi watafaidika na masuala ya kupata udahili wa moja kwa moja kushughulikiwa suala la Visa na kusindikizwa mpaka chuoni ambapo kuna mfumo wa uangalizi upande wa matokeo na maudhurio aliongeza mkurugenzi mtendaji wa GEL.


Katika kujibu baadhi ya maswali ya wandishi wa Habari alisema wanafunzi watakuwa wakiomba kupitia online  na kwa mfumo wa central admission system ambao tayari marekebisho yake yameshakamilika ,na kuhusu vyuo kuna baadhi vitakavyopewa kipaumbele kwa nchi za Ukraini,India, china, Canada, U.S.A ,Malaysia na Uingereza na mikopo hiyo itakuwa kwa ngazi za diploma mbaka shahada ya uzamili.


Katika kutimisha suala hilo Mr Mollel alisisitiza siku ya uzinduzi wa programu hiyo ambayo ni jumapili ya Tarehe 3 novemba 2013 katika ukumbi wa hotel ya serena.














Share