Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

Global sasa yamaliza Kilio cha Wazazi wanaosomesha watoto nje ya nchi

Mkurugenzi Mtendaji Wa Global Education Link, Mr Abdulmalik S. Mollel akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mikopo Kwa Wanaosoma Vyuo Vya Nje Ya Nchi.


Global sasa yamaliza kilio cha Wazazi wanaosomesha Watoto Nje Ya Nchi.

ASILIMIA 99 ya wazazi wanaosomesha watoto wao vyuo vya nje ya nchi wamekuwa wakishindwa kulipia ada ya masomo yao kwa mkupuo, kutokana na hali ya kiuchumi ikilinganishwa na ada kuwa kubwa katika vyuo hivyo. 

Hayo yalisemwa jana Novemba 3,2013 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link Mr Abdulmalik S. Mollel wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vya Nje ya Nchi, kwa kushirikiana na Benki ya Afrika(BOA Bank).


Mollel amesema kuwa baada ya kusikia kilio cha wazazi hao ikilinganishwa na hali ya kiuchumi kuwa sio nzuri kwa baadhi ya Watanzania huku wananfunzi wakiwa na nia nzuri na vigezo vya kuendelea na masomo lakini gharama kubwa zinawafanya kukosa fursa hizo za kusoma nje ya nchi.


“Unajua sisi kama Global tumesikia kilio cha Wazazi hao ambao wana nia ya kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi lakini kutokana na masharti ni lazima mzazi alipe fedha hizo za ada kwa wakati mmoja jambo ambalo limewawia vigumu kulipa kwa wakati mmoja kwahiyo tukaona tuanzishe programu hii ya kuwakopesha ili waweze kufikia malengo yao na ndoto za watoto wao,”alisema Mollel.


Aliongeza kuwa kuna baadhi ya kozi ambazo hazipatikani hapa nchini badala yake zinapatikana nje ya nchi huku gharama zake zikionekana kuwa kubwa na kuwashinda wazazi ingawa wanakuwa na nia ya kuwapatia watoto wao elimu ya kozi hizo lakini wanashindwa.


Baadhi ya kozi hizo ni pamoja na uhandisi wa mafuta,kozi za ndege yaani rubani,upasuaji wa ubongo na kozi nyingine ambazo hazitolewi nchini Tanzania na kwamba kwa sasa kilio hicho kinakaribia kuisha kama sio kupungua kutokana na mikakati ya Kampuni ya Global kuhusu elimu ya vyuo vya nje ya nchi.


Amewaomba wazazi wote ambao wana wanafunzi wenye vigezo vya kuweza kuomba nafasi za vyuo vya nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kwani suala la kushindwa kulipa ada sio tatizo tena.


Serikali imeyataka makampuni kuiga mfano wa Global.




Naibu Katibu Mkuu, Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw.Zuberi M.Samataba, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mikopo Kwa Wanaosoma Vyuo Vya Nje Ya Nchi.


SERIKALI imeyataka mashirika na makampuni binafsi kuiga mfano wa Kampuni ya Global Education Link Limited katika kusaidia masuala mbalimbali likiwemo suala la elimu ili kuipunguzia serikali mzigo wa kufanya kila jambo.


Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es salaam  na Naibu Katibu Mkuu Ofisi Waziri Mkuu Tamisemi Zuberi Samataba wakati wa uzinduzi wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi na kwamba kitendo cha Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) ni kitendo cha kuigwa na baadhi ya makampuni, mashirika na Taasisi binafsi katika kuinua elimu nchini.


“Kusema ukweli kampuni hii ni mfano wa kuigwa katika suala la kuwawezesha Watanzania kupata elimu nje ya nchi maana hata mimi ni shahidi mwanangu wa kwanza anayesoma nje ya nchi alisaidiwa na Global kwahiyo kitendo hiki kinatufanya kushirikiana kwa ukaribu zaidi kuhakikisha kampuni hii inaendelea kuwawezesha Watanzania kupata elimu nje ya nchi,”alisema Samataba.


Samataba alisema kuwa kuna watoto wengi wenye uwezo mzuri kimasoma lakini uwezo wa kupata elimu ya juu limekuwa tatizo kubwa na ikilinganishwa na upatikanaji wa baadhi ya kozi hapa nchini sio kozi zote zinapatikana hapa jambo ambalo linamlazimu mzazi kumtafutia mwanaye kozi hizo nje ya nchi lakini gharama zake zinakuwa juu na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake.



Samataba amesema kuwa baada ya kuzindua mpango huo wazazi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanajisajili ili kuweza kuwapatia watoto wao elimu nje ya nchi zikiwemo kozi ambazo hazipatikani ndani ya nchi.


TCU yawatahadharisha Watanzania juu ya kupata vyuo bora nje ya nchi






 Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), Profesa Magishi Nkwabi Mgasa,akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mikopo Kwa Wanaosoma Vyuo Vya Nje Ya Nchi.



TUME ya vyuo vikuu Tanzania (TCU),imewatahadharisha Watanzania kuwa makini wanapotafuta nafasi za masomo katika vyuo vya nje ya nchi badala yake wakapate ushauri katika Tume hiyo pamoja na mawakala wa vyuo hivyo waliopo Tanzania.


Hayo yalisemwa Novemba 3, 2013 Jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Magishi Nkwabi wakati wa uzinduzi wa Programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya nje ya nchi iliyozinduliwa Novemba 3, 2013.


Programu hiyo inafadhiliwa na Kampuni ya Global Education Link Limited chini ya Mkurugenzi wake Abdulmalik Mollel ambapo wanafunzi wanaosoma nje ya nchi wataweza kukopeshwa baada ya kupata chuo na kutimiza vigezo.


Nkwabi alisema kuwa kuna baadhi ya vyuo nje ya nchi havitambuliki hapa nchini baada ya mwanafunzi kumaliza masomo yake katika chuo ambacho hakitambuliwi na TCU ni kama vile mwanafunzi amepoteza muda wake bure na kwamba kwa sasa kutokana na jitihada za kampuni ya Global suala la udanganyifu litaweza kuisha.


“Napenda kuwaambia wazazi pamoja na wanafunzi kuweni makini maana kuna baadhi ya vyuo nje ya nchi havitambuliwi na TCU,kwahiyo tayari kuna fursa hii ya Global itumieni ili waweze kuwaelekeza na kuwasaidi namna ya kupata vyuo vilivyo bora na kutambuliwa na TCU,”alisema Profesa Nkwabi.


Alisema kuwa Global ni kampuni ambayo wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu sana na kupewa ushauri katika masuala ya vyuo vya nje ya nchi na kwamba kwa sasa kampuni hiyo inaonekana kufanya vizuri na sasa imeleta mpango ambao ni ukombozi kwa Watanzania na kuwaomba kutumia fursa hii kutimiza ndoto zao katika elimu.




Wizara ya Elimu yaipongeza Global


 Mkurugenzi Wa Elimu Ya Juu, Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi, Profesa Sylivia S. Temu, akizindua rasmi Programu Ya Mikopo Kwa Wanafunzi wa vyuo vya nje ya nchi.





  Mkurugenzi Wa Elimu Ya Juu, Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi, Profesa Sylivia S. Temu,akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mikopo Kwa Wanaosoma Vyuo Vya Nje Ya Nchi.



WIZARA  ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeipongeza Kampuni ya Global Education Link Limited kutokana na mpango wake wa kuanzisha mpango wa kuwapatia mikopo wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi.


Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Profesa Sylivia Temu wakati akizindua programu hiyo Novemba 3, 2013 Jijini Dar es salaam na kwamba serikali haina budi kuwapongeza hasa katika suala la elimu kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.


“Napenda kuipongeza Kampuni ya Global kwa niaba ya Wizara ya elimu, maana hili ni suala kubwa sana la kuwakopesha wanafunzi wanaosoma nje ya nchi ni kitendo cha kuigwa na makampuni mengine hapa nchini maana elimu ndiyo kila kitu kuna baadhi ya wazazi wanapenda kuwasomesha watoto wao nje ya nchi lakini hali ya uchumi hairuhusu pamoja na kuwa na vigezo, hongereni sana,”alisema ProfesaTemu.


Aliahidi kutoa ushirikiano kwa kampuni ya Global ili mpango huo usiishie hewani badala yake uwe mkombozi kwa Watanzania wote wenye nia ya kupata elimu nje ya nchi na kwamba Taifa lenye watu wasomi ndilo linaliofanikiwa kiuchumi na katika mambo mengine.


Aliwaomba Wananchi kutumia fursa hii kwa wenye vigezo kupata mikopo ili kuweza kupata elimu nje ya nchi hasa kwa kozi ambazo hazipatikani hapa nchini na kuweza kuzipata katika vyuo hivyo vinavyotoa kozi hizo.






Share