Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

TLTC YAIKABIDHI SEKONDARI URAMBO VITABU VYA MILIONI 5.3/-

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Urambo, Shadrack Yomba (kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Kampuni ya Tumbaku nchini(TLTC), Sylivester Kapungu, wakigawa msaada wa vitabu vya kiada kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Usisya.

Kampuni ya Tumbaku nchini (TLTC), imekabidhi vitabu vyenye thamani ya Sh. milioni 5.3 kwa Shule ya Sekondari Usisya iliyopo katika Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.



Akipokea msaada huo wa vitabu, Ofisa Elimu wa wilaya hiyo, Grace Monge, alisema shule za sekondari wilayani Urambo zina uhaba mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi.

Monge ambaye alikuwa amefuatana na na mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya Urambo, Shadrack Yomba, alisema kutokana na  uhaba huo, wamelazimika kuajiri kwa muda walimu waliomaliza kidato cha sita ambao walikuwa wanachukua masomo ya sayansi.

Pamoja na kuwashukuru TLTC, ambao ni wanunuzi wakubwa wa tumbaku wilayani Urambo na wilaya nyingine zinazozalisha zao hilo, Monge alizitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa TLTC katika kusaidia miradi ya elimu ili kukidhi matakwa ya elimu katika wilaya ya Urambo.

Sekondari ya Usisya ambayo iliyofunguliwa Aprili, 2007, kama zilivyo shule nyingine zilizojengwa kwa nguvu za wananchi maarufu kama sekondari ya kata mkoani Tabora, zina matatizo ya walimu, nyumba za
makazi kwa wafanyakazi na maabara.

Akishukuru kwa msaada huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Urambo, Yomba, alisema halmashauri yake inajivunia uwapo wa
kampuni ya TLTC katika mkoa huo kutokana na kujitolea kuwasaidia mara kadhaa.

“Siku zote tunafikia malengo yetu kwa kasi kuliko inavyotarajiwa kwa sababu ya ushirika wenu kwetu. Siku zote tutakuwa tunawashukuru kwa misaada yenu,” alisema.

Akikabidhi vitabu hivyo, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TLTC, Sylivester Kapungu, alisema msaada huo umetolewa kwa kuzingatia sera za
kampuni hiyo za kushirikiana na serikali katika sekta za elimu, afya na maji.

“Tunaamini kuwa elimu bora ina uhusiano na mazingira hasa ujenzi wa nyumba bora, walimu bora na vitabu. Kama una wanafunzi wazuri; lakini
hawana vitabu, utapanda mbegu lakini hutapata mavuno mzuri,” alisema.

Mwalimu Mkuu wa Skondari ya Usisya, Herman Shija, alisema shule yake imekuwa haifanyi vyema katika masomo ya sayansi kutokana na kukosa walimu  wa sayansi na vitabu.

Alisema msaada waliopewa ni ufunguo mkubwa wa mafanikio kwao.

 
Share