Mkurugenzi mtendaji wa GEL,Abdulmalik Mollel akiwa katika uwasilishaji wa mada kwa wanafunzi wa FORM 5 na FORM 6,St. Marie Goreti Secondary School iliyopo Moshi mjini.
Abdulmalik Mollel, akitoa elimu juu ya uchaguzi wa kozi zenye manufaa kwa wanafunzi na taifa letu.Na kuwaandaa wanafunzi juu ya maamuzi yao katika elimu na katika vyuo watakavyochagua.
Wanafunzi wa A level wakifuatilia mada za GEL,juu ya ushauri katika kozi nzuri za kusomea, vigezo vya kupata udahili wa vyuo vya nje ya nchi.
Mkurugenzi wa GEL akiendelea kuwaelimisha wanafunzi,wapate kujua nini cha kufanya baada ya kumaliza masomo yao ya kidato cha sita, pia kufahamu namna ya kupata udahili wa vyuo vya nje kwani wanafunzi wengi wa hapa nchini wanaamini kuwa udahili wa vyuo vya nje ni gharama kubwa sana.GEL wanakurahisishia namna ya kwenda kusoma nje na kwa gharama nafuu.
Abdulmalik Mollel akijadiliana na wanafunzi juu ya changamoto wanazokutana nazo katika masomo yao na namna watakavyoweza kukabiliana na hizo changamoto.