
Ileje. Halmashauri ya Wilaya ya Ileje imetumia kiasi Sh35.8 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara rafiki ili kuondokana na tatizo lililokuwa linawakabili katika mafunzo ya vitendo kwa masomo ya Sayansi.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule
aliyasema hayo wakati wa makabidhiano ya maabara hizo na Kampuni ya
Mlenterprises (LTD), na kuongeza kuwa tatizo la wanafunzi kusoma bila
mafunzo ya vitendo litapungua.
Senyamle aliongeza kuwa halmashauri hiyo
inaishukuru serikali kwa kuweza kuwapatia fedha hizo kwa kuwa imesaidia
kuondokana na tatizo ambalo lilikuwa linaikumba wilaya hiyo kwa muda
mrefu.
PICHA: MWANANCHI
PICHA: MWANANCHI