Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

PROFILE ZA WAGOMBEA NCHINI KENYA.

Raila Amollo Odinga
  Raila Odinga alizaliwa Januari tarehe 7 mwaka 1945 Magharibi mwa Kenya mkoa wa Nyaza. Raila ni waziri mkuu wa kwanza wa Kenya , wadhifa ulioundwa kufuatia mkataba wa kitaifa ulioafikiwa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008 kama ishara ya kugawana mamlaka.

Alitia saini mkataba wa kugawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki ili kumaliza ghasia za miezi miwili zilizokumba nchi baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata.

Raila mwenye umri wa miaka 68 wa chama cha ODM ingawa kwa sasa anagombea urais kwa muungano wa CORD, ameamua kushirikiana na makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, ambaye pia alikuwa hasimu wake miezi miwili tu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2007.


 Uhuru Muigai Kenyatta

 Naibu waziri mkuu wa Kenya tangu mwaka 2008, Uhuru Kenyatta, alizaliwa tarehe 26 Oktoba mwaka 1961 kwa Mama Ngina na Mzee Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Kenya, kati ya mwaka 1964-1978, na akaitwa "Uhuru", neno la Kiswahili linalomaanisha ukombozi kutoka kwa wakoloni.

Mrithi wa mashamba makubwa Kenya, anatajwa kuwa nambari 23 katika orodha ya watu matajiri zaidi Afrika akiwa na thamani ya dola milioni miatano.

Uhuru, anayejulikana na wafuasi wake kama "Njamba" neno la Kikikuyu, linalomaanisha, Shujaa, ni mgombea wa urais wa muungano wa Jubilee, ambao ni muungano wa vyama vya TNA chake Kenyatta, (URP) na (Narc). 


Mgombea mwenza wake ni William Ruto wakisaidiana na Charity Ngilu,Mwalimu wake wa siasa ambaye ni Rais mstaafu, Daniel Moi alimuingiza katika siasa kwa mara ya kwanza na kumpendekeza kuwa mgombea wa urais licha ya kutokuwa na uzoefu wa kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2002.



 Wycliffe Musalia Mudavadi

Alizaliwa tarehe 21 Septemba mwaka 1960 Magharibi mwa Kenya kutoka jamii ya waluhya.
Mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 52, na ambaye siasa zake hazichangamshi sana ikilinganishwa na wanasiasa wengine, na wengi wakisema ni kwa sababu ya alivyolelewa na wazazi wake katika misingi ya kidini sana.

Mudavadi alimteua aliyekuwa mbunge Jeremiah Kioni kutoka mkoa wa kati kama mgombea mwenza wake katika chama chao cha muungano wa AMANI.

Vyama vilivyo katika muungano huo, ni kumi na tatu kikiwemo chama cha KANU chake rais mstaafu Daniel Moi. Wadadisi wanasema kuwa kuibuka kwa chama hiki huenda kukasababisha duru ya pili, ya uchaguzi na wachanganuzi wanasema Muungano wa AMANI utakuwa changamoto kwa azma ya Kenyatta na Raila.

Mudavadi alikuwa mmoja wa mawaziri wakuu wawili walioteuliwa katika serikali ya Muungano kati ya Raila na Kibaki kufuatia mkataba wa amani uliofikiwa baada ya ghasia za uchaguzi.

Alikuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2007 kabla ya kujiuzulku ili kugombea urais mwaka huu.

Mudavadi pia alikuwa mgombea mwenza wa Uhuru katika uchaguzi wa mwaka 2002, lakini hata akashindwa katika eneobunge lake.


 Martha Wangari Karua


Alizaliwa tarehe 22 Septemba mwaka 1957 mkoa wa kati. Na yeye ndiye mgombea wa pekee mwanamke katika uchaguzi huu. Aliajiriwa kama hakimu akiwa na umri wa miaka 24 kabla ya hata kuwa mbunge miaka kumi baadaye.
Mgombea wa muungano wa National Rainbow Coalition (Narc-Kenya), Karua alimteua mwanauchumi Augustine Chemonges Lotodo kama mgombea mwenza wake. Lotodo pia amewahi kuwa mbunge katika bunge la Afrika Mashariki

Karua mwenye umri wa miaka 55, alikuwa mwanachama wa upinzani ambao walipigania siasa za vyama vingi nchini Kenya mapema miaka ya tisini chini ya utawala wa rais mstaafu Daniel Moi aliyekua anaongoza kimabavu chini ya chama kimoja.

Mkereketwa wa demokrasia na maswala ya wanawake nchini Kenya, Karua alihusika na kupigania haki za wanawake kwa kutaka uungwaji mkono katika maswala yanayowahusisha wanawake wenyewe.

Karua alikuwa mfuasi mkubwa wa rais Mwai Kibaki na sera zake hadi tarehe sita Aprili mwaka 2009 wakati alipojiuzulu kama waziri wa sharia, akielezea kuwa kazi yake ilikuwa inaingiliwa sana na baadhi ya maafisa wakuu serikalini.

Aliongoza upande wa serikali wakati wa mapatano kati ya Raila Odinga na Kibaki ili kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi.

Pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa maji aliyepigia debe sana sheria ya maji ya mwaka2002 ambayo ilichochea mageuzi katika sekta hiyo.

Peter Kenneth

Peter Kenneth alizaliwa tarehe 27 Novemba mwaka 1965 na anatoka mkoa wa kati. Ndiye mgombea wa kwanza asiye na jina asilia la kiafrika.
Akiwa ndiye mgombea mwenye umri mdogo sana, anasisitiza kuwa , yeye kama kiongozi mwenye mchanganyiko wa makabila, atahakikisha kuwa ukabila ambalo ni tatizo sugu Kenya , unamalizika.

Akiwa mdogo wa umri ikilinganishwa na wagombea wengine, Kenneth mwenye umri wa miaka 47, alipigiwa debe sana kwa namna alivyoleta maendeeo katika eneo bunge lake.

Kama naibu waziri, katika serikali ya Rais Kibaki,Kenneth anagombea urais kwa muungano wa EAGLE, ambao umewaleta pamoja waliokuwa wanafunzi wenza katika shule ya sekondari ya Starehe . 

Mgombea mwenza wa Peter Kenneth ni meneja mkuu katika kampuni ya huduma za simu ya Safaricom.

Kenneth alikuwa mgombea wa kwanza wa urais kuzindua ruwaza yake ambayo ilitaja sekta 13 ambazo atazipatia kipaombele ikiwa atashinda urais.
Share