Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WAZAZI KIKWAZO CHA ELIMU,KIBAHA

 WAZAZI waliopo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, wametajwa kuwa wanachangia kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani hapa. Hali hii inakuja kutokana na kuwepo kwa mwamko mdogo kuhusu dhana ya uchangiaji wa maendeleo katika sekta ya elimu.
Madai hayo yaliibuliwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Hajjat Halima Kihemba, alipokuwa akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu.

Kikao hicho kiliandaliwa na halmashauri hiyo kwa lengo la kujadili jinsi ya kuboresha elimu pamoja na kuweka mikakati ya kupambana na changamoto zilizopo.

Kihemba, alisema wazazi wengi wilayani Kibaha wamekuwa na kasumba ya kugoma kuchangia maendeleo ya elimu huku wengine wakidai kuwa uwezo wao ni mdogo.

"Tumekuwa tukipata shida sana na baadhi ya wazazi kwa kuwa bado hawana mwamko wa elimu, jambo ambalo linapelekea wengi wao kushindwa kuchangia katika maendeleo ya elimu.

“Hata pale ambapo wanalazimika kwani mara nyingi wamekuwa wakisema wao ni maskini, hali hii inazidi kukwamisha miradi mingi ya maendeleo hususan katika sekta ya elimu,” alisema.

Kihemba aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wameanza kuweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wazazi ili waweze kuelewa umuhimu wa kuchangia katika sekta hiyo.

Kihemba alisema pamoja na kuwepo kwa mwamko mdogo wa wazazi katika kuchangia elimu lakini pia alitaja changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katika sekta hiyo.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni mazingira duni ya kazi kwa walimu, upungufu wa miundombinu ya shule kama vile madarasa, vitabu, maabara na maktaba.

Alisema pamoja na changamoto hizo lakini halmashauri hiyo kwa mwaka 2012 iliweza kufanya vyema kwa upande wa Elimu ya Msingi kwa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa.

Hata hivyo, kikao hicho kiliwajumuisha wanasiasa, wenyeviti wa bodi za shule na kamati zake, wakuu wa shule, walimu wakuu, waratibu elimu wa kata, wafadhili wa elimu na wakuu wa idara.
Share