Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WANAFUNZI UDSM WAMBANA WAZIRI MKUU WA DENMARK.

     Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji naUwezeshaji),  Dk. Mary Nagu.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu ccha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na kampasi zake wamembana Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa ziara yake ya kukitembelea chuo hicho.

Wanafunzi hao walimtaka Waziri Mkuu huyo kueleza madhumuni ya misaada mbalimbali inayotolewa na serikali yake nchini ikiwamo ya elimu iwapo inatolewa ili kuinua kiwango cha elimu au la.



Kutolewa kwa hoja hiyo kunafuatia wnafunzi hao kudai kuwa iwapo Serikali ya Denmark ingekuwa  ikiisaidia Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu, elimu nchini isingedidimia wakitolea mfano wa matokeo mabaya ya mtihani wa kiadato cha nne mwaka jana.

Schmidt alisema kuwa serikali yake imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta ya elimu kwa muda mrefu, lakini kwa sehemu kubwa ilikuwa ikilenga wanafunzi wa elimu ya juu wakiwamo wale wanaochukua shahada za uzamili kwa kutoa ufadhili na ujenzi wa miundombinu katika chuo hicho.

Katika mkutano huo uliojumuisha jumuiya ya chuo hicho, Schmidt alisisitiza umuhimu wa elimu akisema kwamba ni ufunguo wa maendeleo ya uchumi kwa taifa lolote duniani.

Alisema nchi husika inapaswa kuwa na mipango ya makusudi na ya muda mrefu katika eneo la elimu huku akisisitiza kupiga vita mimba kwa watoto wa shule ili kundi hilo liweze kupatiwa elimu kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa watoto wa kiume.

Katika ziara hiyo, aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, huku akiwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwani wao ndio viongozi watarajiwa.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema ziara ya Waziri Mkuu huyo chuoni hapo ina umuhimu mkubwa kwani ni moja ya uthibitisho wa ushirikiano uliokuwapo kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Denmark.

Profesa Mukandala aliongeza kuwa UDSM kimekuwa na ushirikiano na serikali ya Denmark kwa muda mrefu na kwamba kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maedneleo (Danida) imefanikiwa kuendeleza baadhi ya miundombinu ya majengo chuoni hapo ikiwamo Shule ya Biashara.

Schmidt alitembelea baadhi ya majengo ambayo Denmark imeshiriki katika kuyaedeleza kiujenzi pamoja na mti maarufu chuoni hapo unaojulikna kama mti wa mdigrii.
 
Share