Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WASIOAMINI MATOKEO KIDATO CHA NNE(4) WAKATISHWA TAMAA

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), limeeleza kuwa mara nyingi ukataji rufaa na usahihishaji upya wa mitihani hiyo, matokeo yamekuwa hayabadiliki kutokana na umakini wa usahihishaji.

Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kuhusu matokeo ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana, waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya.

Kwa mujibu wa Nchimbi, mpaka sasa wanafunzi 530 wamekata rufaa ya kutaka kusahihishiwa upya mitihani yao ya kidato cha nne, na matokeo ya wanafunzi saba tu ndiyo yaliyobadilika.Alisema katika wanafunzi hao saba ambao matokeo yao yamebadilika, mmoja matokeo yake amejikuta akipata alama F badala ya D aliyokuwa ameikatia rufaa kwenye somo la Kiingereza.

Akizungumza tathmini ya ukataji rufaa na usahihishaji upya wa mitihani hiyo, Nchimbi alisema : "Kwa sasa siwezi kukupa tathmini ya idadi ya walioomba kusahihishiwa upya kama imepanda au la."

"Lakini hata ukiangalia waliosahihishiwa kwa waliojitokeza katika awamu ya kwanza, watahiniwa saba ambao matokeo yao yamebadilika ni wengi, kwani miaka ya nyuma haifiki hata asilimia moja ya watu wanaoomba," alisema.

Hata hivyo, Nchimbi alisema bado Baraza hilo linatoa nafasi kwa wanafunzi wengine kuomba kusahihishiwa upya mitihani yao, na kuwa shughuli hiyo itafungwa rasmi April 18 mwaka huu.



  

Share