Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WALIMU WAWEKA REHANI KADI ZA ATM.

                        Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadege
Walimu zaidi ya 300 katika wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wameweka rehani kadi za mashine za kutolea fedha benki(ATM) baada ya kukopa kwa watu binafsi.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadege alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa kawaida wa mwaka wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos) cha walimu wilayani hapa kinachojumuisha pia wanachama kutoka wilaya ya Momba.

Alisema ni jambo la kusitikisha kwa walimu wanaoaminiwa na jamii kuwa werevu kujiingiza katika mikopo ya namna hiyo inayowalazimu kutoa pia namba zao za siri na kuruhusu wakopeshaji kwenda kujichukulia fedha benki mara mishahara inapotoka.
"Walimu wametoa kadi wakakabidhi na namba zao za siri hivyo mkopeshaji anaamua mwenyewe akatoe shilingi ngapi kwenye akaunti husika. Sijui walimu hawa wakitapeliwa na mkopeshaji wa namna hii watamfikisha katika chombo gani cha sheria kwa kuwa hakuna mkataba wowote waliowekeana", alihoji Dk Kadege.

Alisema matokeo ya mikopo ya aina hiyo imekuwa ni walimu kushindwa kutimiza wajibu wao wa kufundisha badala yake wanautumia muda wa vipindi kufanya kazi mbadala, ikiwemo kuendesha bodaboda.

Alisema hali hiyo inatokana na walimu kuchukua mikopo zaidi ya mishahara yao,kwani kupitia mpango huo wa kukopeshana kienyeji, haupo utaratibu wa ukomo wa mkopo kama ilivyo kwa mikopo inayotolewa kwa taratibu stahili.

Mkuu huyo wa wilaya aliusihi uongozi wa Saccos ya walimu kuhimiza walimu kujiunga na chama hicho waweze kukopa kwa taratibu zinazotakiwa na kuepuka mikopo ya kitapeli ambayo haiwezi kuwaletea manufaa kutokana na riba kubwa wanayotozwa.

Mmoja wa maofisa wa Benki ya CRDB mkoani Mbeya, Alpha Manota aliwasihi wateja wa benki kuacha tabia ya kuamini kila mtu katika jamii inayowazunguka kwa kutoa kadi ya ATM na namba ya siri.

Share