Pages

Welcome to GLOBAL EDUCATION LINK. STUDY ABROAD through US. WE Admit YOU to Overseas Universities, We give YOU right Information, WE Advice on Course Selection, WE Guide YOU On Your CAREER, WE Guide YOU on University SELECTION, WE Assist YOU on YOUR Visa Process. JOIN US NOW OR CALL US ON 0656 200 200 for MORE Information. WELCOME TO FEEL THE DIFFERENCE.

WASICHANA WENGI WADAHILIWA ELIMU YA JUU.

Mhe. Ummy Mwalimu-Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.


Kiwango cha udahili  wa wanafunzi wa kike  kujiunga na elimu ya vyuo vya  juu kimeongezeka kutoka wanafunzi 49,959 mwaka 2010/11 hadi 60,592 (asilimia 19).


Aidha,  katika shule za sekondari umeongezeka kutoka wanafunzi 728,528 hadi 802,554 ikiwa (asilima 9.2) ukiwa ni uwiano wa wanafunzi wa kike na wa kiume kuwa asilimia 44.8.


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa wakati akizumgumzia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo.


Alisema vitendo vya ukatili kama ukeketaji vimepungua kutoka asilimia 18 hadi asilimia 15 kwa mwaka 2010 wanatarajia kiwango hicho kitapungua zaidi ifikapo mwaka 2015.


Mwalimu alisema  wanawake wamewezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na mikopo yenye masharti nafuu kupitia benki ya wanawake Tanzania hadi kufikia Juni 2012 ilitoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 1.2 kwa wanawake 5,270 na wanaume1,157.
 

Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Uelewa wa masuala  ya jinsia katika jamii,ongeza kasi’
Share