Kamanda Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwa kushirikiana na mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Nge, wamevamia ofisi za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na kumlewesha kwa chakula kinachodaiwa kuchanganywa na dawa za kulevya mlinzi wa kampuni anayelinda katika ofisi hizo na kuvunja milango kisha kupora nyaraka na mali mbalimbali.
Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea usiku wa kumkia jana.
Alivitaja vitu vilivyoibwa kuwa ni kompyuta tano, Laptop mbili pamoja na CPU moja vyenye thamani ya Sh milioni 14.
Alisema walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Nge, Said Abdalah na Kasimu Salehe walikuwa zamu ya kulinda katika ofisi hizo.
Alisema ilipofika nyakati za usiku Said alimpa mwenzake chakula
kinachosadikiwa kuchanganywa na jana asubuhi alikutwa akiwa amelaa bila
kujitambua.
Kamanda Kenyela alisema baada ya mlinzi huyo kufanya kitendo hicho, alitoroka.
NIPASHE lilifika eneo la la tukio na kushuhudia baaddhi ya milango
ikiwa imevunjwa kwa vitu vizito. Pia kabati la kuhifadhia nyaraka muhimu
lilikatwa kwa kutumia moto wa gesi huku ofisi zingine zikiwa
zimepekuliwa na nyaraka kutupwa ovyo.
Taarifa zinaeleza kuwa mlinzi aliyempa mwenzake chakula hicho
kinachosadikiwa kuwa na dawa za kulevya aliajiriwa Februari 26, mwaka
huu na hafahamiki anakoishi.
Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Nge, Pius Mgaya, alisema waliingia mkataba ya ulinzi na TCU Machi 1, mwaka huu.
Alisema mlinzi wao aliyekimbia baada ya kufanya kitendo hicho
alidhamilia kwa muda mrefu kutokana na baada ya tukio hilo alibadilisha
nguo za kazi na kuvaa za kiraia pamoja na kuacha bunduki ikiwa na risasi
tano.
Afisa Habari wa TCU, Edward Mkaku, alisema ofisi saba zilivunjwa na baadhi ya vitu zikiwamo kompyuta kuchukuliwa.
Alisema kutokana na tukio hilo, kuna haja TCU kuweka mitambo ya
kuhifadhi matukio yote yanayotokea katika taasisi hiyo kwa sababu ni
tukio la pili TCU kuvamiwa inavamiwa na majambazi katika kipindi cha
mwaka mmoja.
Juni 25, mwaka jana ofisi hizo zilivamiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwamo fedha na kompyuta