Raila Amollo Odinga
Raila Odinga alizaliwa Januari tarehe 7 mwaka 1945 Magharibi mwa
Kenya mkoa wa Nyaza. Raila ni
waziri mkuu wa kwanza wa Kenya , wadhifa ulioundwa kufuatia mkataba wa
kitaifa ulioafikiwa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008
kama ishara ya kugawana mamlaka.Raila mwenye umri wa miaka 68 wa chama cha ODM ingawa kwa sasa anagombea urais kwa muungano wa CORD, ameamua kushirikiana na makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, ambaye pia alikuwa hasimu wake miezi miwili tu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Uhuru Muigai Kenyatta
Naibu waziri mkuu wa Kenya tangu mwaka 2008, Uhuru Kenyatta, alizaliwa tarehe 26 Oktoba mwaka 1961 kwa Mama Ngina na Mzee Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Kenya, kati ya mwaka 1964-1978, na akaitwa "Uhuru", neno la Kiswahili linalomaanisha ukombozi kutoka kwa wakoloni.
Uhuru, anayejulikana na wafuasi wake kama "Njamba" neno la Kikikuyu, linalomaanisha, Shujaa, ni mgombea wa urais wa muungano wa Jubilee, ambao ni muungano wa vyama vya TNA chake Kenyatta, (URP) na (Narc).
Mgombea mwenza wake ni William Ruto wakisaidiana na Charity Ngilu,Mwalimu wake wa siasa ambaye ni Rais mstaafu, Daniel Moi alimuingiza katika siasa kwa mara ya kwanza na kumpendekeza kuwa mgombea wa urais licha ya kutokuwa na uzoefu wa kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2002.
Wycliffe Musalia Mudavadi
Alizaliwa tarehe 21 Septemba mwaka 1960 Magharibi mwa Kenya kutoka jamii ya waluhya.
Mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 52, na
ambaye siasa zake hazichangamshi sana ikilinganishwa na wanasiasa
wengine, na wengi wakisema ni kwa sababu ya alivyolelewa na wazazi wake
katika misingi ya kidini sana.Vyama vilivyo katika muungano huo, ni kumi na tatu kikiwemo chama cha KANU chake rais mstaafu Daniel Moi. Wadadisi wanasema kuwa kuibuka kwa chama hiki huenda kukasababisha duru ya pili, ya uchaguzi na wachanganuzi wanasema Muungano wa AMANI utakuwa changamoto kwa azma ya Kenyatta na Raila.
Mudavadi alikuwa mmoja wa mawaziri wakuu wawili walioteuliwa katika serikali ya Muungano kati ya Raila na Kibaki kufuatia mkataba wa amani uliofikiwa baada ya ghasia za uchaguzi.
Alikuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2007 kabla ya kujiuzulku ili kugombea urais mwaka huu.
Mudavadi pia alikuwa mgombea mwenza wa Uhuru katika uchaguzi wa mwaka 2002, lakini hata akashindwa katika eneobunge lake.
Martha Wangari Karua
Alizaliwa tarehe 22 Septemba mwaka 1957 mkoa wa kati.
Na yeye ndiye mgombea wa pekee mwanamke katika uchaguzi huu. Aliajiriwa
kama hakimu akiwa na umri wa miaka 24 kabla ya hata kuwa mbunge miaka
kumi baadaye.
Mgombea wa muungano wa National Rainbow
Coalition (Narc-Kenya), Karua alimteua mwanauchumi Augustine Chemonges
Lotodo kama mgombea mwenza wake. Lotodo pia amewahi kuwa mbunge katika
bunge la Afrika MasharikiMkereketwa wa demokrasia na maswala ya wanawake nchini Kenya, Karua alihusika na kupigania haki za wanawake kwa kutaka uungwaji mkono katika maswala yanayowahusisha wanawake wenyewe.
Karua alikuwa mfuasi mkubwa wa rais Mwai Kibaki na sera zake hadi tarehe sita Aprili mwaka 2009 wakati alipojiuzulu kama waziri wa sharia, akielezea kuwa kazi yake ilikuwa inaingiliwa sana na baadhi ya maafisa wakuu serikalini.
Aliongoza upande wa serikali wakati wa mapatano kati ya Raila Odinga na Kibaki ili kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi.
Pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa maji aliyepigia debe sana sheria ya maji ya mwaka2002 ambayo ilichochea mageuzi katika sekta hiyo.
Peter Kenneth
Peter Kenneth alizaliwa tarehe 27 Novemba mwaka 1965
na anatoka mkoa wa kati. Ndiye mgombea wa kwanza asiye na jina asilia la
kiafrika.
Akiwa ndiye mgombea mwenye umri mdogo sana,
anasisitiza kuwa , yeye kama kiongozi mwenye mchanganyiko wa makabila,
atahakikisha kuwa ukabila ambalo ni tatizo sugu Kenya , unamalizika.Kama naibu waziri, katika serikali ya Rais Kibaki,Kenneth anagombea urais kwa muungano wa EAGLE, ambao umewaleta pamoja waliokuwa wanafunzi wenza katika shule ya sekondari ya Starehe .
Mgombea mwenza wa Peter Kenneth ni meneja mkuu katika kampuni ya huduma za simu ya Safaricom.
Kenneth alikuwa mgombea wa kwanza wa urais kuzindua ruwaza yake ambayo ilitaja sekta 13 ambazo atazipatia kipaombele ikiwa atashinda urais.