Wapiga kura katika mtaa wa Kibera.
Foleni za wapiga kura Mombasa.
Foleni za wapiga kura Nairobi.
Raia wa Kenya wameanza shughuli ya kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza unaofanyika chini ya katiba mpya.
Katika uchaguzi huu watamchagua rais pamoja na wawakilishi wa wanawake, magavana, na maseneta wa majimbo 47 ya nchi hiyo.
Katika mji mkuu Nairobi misururu mirefu ya wapigakura ilionekana kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa 12 za Afrika mashariki.
Ushindani mkubwa wa kiti cha urais unatarajiwa kuwa baina ya kiongozi wa muungano wa Cord, Raila Odinga, na yule wa muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta.
Japokuwa tume ya uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo.
Waziri mkuu Raila Odinga
ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera.
Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa
na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa
shwari