WANANCHI wa Kenya leo wanapiga kura kuwachagua viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya kupata Katiba Mpya, ambao unawapambanisha vikali watoto wa waasisi wa taifa hilo ambao sasa ni marehemu.
Uchaguzi wa leo unaelezwa kuwa na kinyang’anyiro 
kikali ambacho hakijawahi kushuhudiwa baina ya wagombea wawili wa urais,
 Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee na Raila Odinga wa Cord.
                
              
Uhuru ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee 
Jomo Kenyatta wakati Raila ni mtoto wa aliyekuwa makamu wa Kenyatta, 
Jaramog Oginga Odinga.
                
              
Mbali na wagombea hao wenye matumaini ya kuingia 
Ikulu kila mmoja, wapo wengine sita – Musalia Mudavadi (UDF), Peter 
Kenneth (Eagle Alliance), Martha Karua (Narc), Mohammed Abduba Dida 
(ARK), Prof James ole Kiyiapi (RBK) na Paul Muite wa Safina.
                
              
Wagombea wote walihitimisha  kampeni zao Jumamosi 
na jana hakukuwa na kampeni kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Kenya. 
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), imesema maandalizi yote
 yamekamilika na vifaa vyote vya kupigia kura vimeshafika katika maeneo 
husika.
                
              
Mwenyekiti wa IEBC, Ahmed Hassan alisema katika 
taarifa yake jana kuwa vituo vitafunguliwa saa 12:00 asubuhi na kufungwa
 saa 1:00 jioni, lakini kama kutakuwa na wapigakura kwenye foleni 
wataendelea hadi watakapokuwa wamemaliza kupiga kura.
                
              
Kwa mujibu wa Hassan, kura zote zitahesabiwa vituoni na matokeo kutumwa kwa njia ya simu.
                
              
Kwenye kampeni zao za lala salama wagombea wenye 
nguvu, Odinga na Kenyatta, wamewahamasisha wapigakura kujitokeza kwa 
wingi na kuwachagua, ili waweze kushinda katika raundi ya kwanza.
                
              
Msukumo huo unatokana na uwezekano wa kura kupigwa
 kwa raundi ya pili Aprili 10, kutokana na uwezekano wa wagombea wote 
wanane kushindwa kufikisha nusu ya kura zote, kwa mujibu wa kura za 
maoni zilizofanyika awali.
                
              
Wakati uchaguzi wa leo umeigharimu Serikali Sh24.9
 bilioni (Sh473.1 bilioni za Tanzania), ule wa marudio unakadiriwa 
kugharimu Sh11.2 bilioni (sawa na Sh212.8 bilioni).
                
              
Uhuru Kenyatta Alisema; 
Nina matumaini kuwa kazi niliyofanya mimi na washirika wangu katika Muungano wa Jubilee, wafanyakazi makini wa chama changu cha TNA na maelfu ya wafuasi wangu, italipa.
                
              Nina matumaini kuwa kazi niliyofanya mimi na washirika wangu katika Muungano wa Jubilee, wafanyakazi makini wa chama changu cha TNA na maelfu ya wafuasi wangu, italipa.
Pia ninatamani uchaguzi wa amani na matumaini 
haya yanazidi hata furaha ya ushindi wa Jubilee. Sitaki tena Kenya 
irejee katika matukio ya 2007/8.
 
