WANAFUNZI 1067 wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wameacha masomo katika miaka minne kutokana na tatizo la mimba na utoro, imeelezwa. Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo Saverina Misinde alisema hali inaendelea kudumaza elimu hasa kwa watoto wa kike.
Alikuwa akitoa mada katika kikao cha wadau wa elimu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Kikao hicho kiliwashirikisha wakuu wa shule, waratibu elimu na wadau wengine kuangalia hali ya elimu katika halmashauri hiyo.
Alisema mwaka 2009 wanafunzi 46 waliacha masomo kwa mimba huku watu waliohusika kufanya vitendo hivyo hawakuchukuliwa hatua za sheria baada ya wazazi kutotoa ushirikiano kwa walimu na vyombo vya dola.
Misinde alisema hakuna hatua madhubuti ambazo zinachukuliwa kuwawajibisha wahusika kwa vile wanapofikishwa mahakamani wanafunzi waliopewa mimba hukataa kutoa ushahidi.Alikuwa akitoa mada katika kikao cha wadau wa elimu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Kikao hicho kiliwashirikisha wakuu wa shule, waratibu elimu na wadau wengine kuangalia hali ya elimu katika halmashauri hiyo.
Alisema mwaka 2009 wanafunzi 46 waliacha masomo kwa mimba huku watu waliohusika kufanya vitendo hivyo hawakuchukuliwa hatua za sheria baada ya wazazi kutotoa ushirikiano kwa walimu na vyombo vya dola.
Alisema mwaka 2009 wanafunzi 331 walikatisha masomo kwa utoro huku lawama pia zikielekezwa kwa wazazi ambao wamekuwa wakiwaona watoto wao wakikaa nyumbani bila kuchukua hatua.
Ofisa elimu huyo alisema mwaka 2010 wanafunzi tisa walipata mimba wakati mwaka 2011 wanafunzi wanane walipata mimba na mwaka 2012 wanafunzi 10 walikumbwa na tatizo hilo huku katika kipindi hicho, wanafunzi 663 walikatisha masomo kwa utoro.
Akichangia katika suala hilo, Ofisa Elimu mstaafu wa Mkoa wa Mara, Nashon Otieno alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi ni jambo kubwa linalohitaji kila mdau kuona kuwa ni changamoto inayohitaji mkakati wa ushirikiano kutoka kwa kila mmoja.
Chanzo: MTANZANIA.