Na Happiness Mnale.
BODI ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB),
imeishauri serikali kufungua vitivo vya taaluma hiyo katika vyuo vyote
nchini.
Bodi hiyo imefikia hatua hiyo, ili kupata wataalamu wa masuala ya majengo watakaoendana na teknolojia na kuziba pengo la uchache wao.
Akizungumza jijini Dar es Saalam jana, Mwenyekiti wa AQRB, Dk. Ambwene Mwakyusa, alisema mpaka sasa kuna wabuni wa majengo na wakadiriaji majenzi wapatao 770 waliosajiliwa kwa nchi nzima.
Dk. Mwakyusa pia alisema kuanzia sasa watafanya msako kwa watu wanaouza ramani bila idhini, kwani sheria iliyokuwa inawabana kuchukua hatua kwa sasa inawalinda.
“Watanzania wengi wanaamini ujenzi ni kitu rahisi, hawajui kujenga ni taaluma, wanaoongoza kwa kujenga kiholela ni watu binafsi,” alisema.
Aidha, Dk. Mwakyusa alitaka serikali iwatumie katika ujenzi wa barabara mbalimbali, ili kufanya ubunifu na hatimaye kupata barabara bora.
Naye Msajili wa AQRB, Jehad Abdalla Jehad, alisema bodi hiyo itaendesha semina endelevu ya 19, jijini Mwanza, kuanzia Machi 14 hadi 15 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Jehad alisema lengo la semina hiyo ni kuwanoa wabunifu majengo na wakadiriaji kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya ujenzi, kubadilishana uzoefu, njia za kudhibiti mabadiliko ya gharama katika sekta ya ujenzi.