Kiwango cha udahili wa wanafunzi wa kike kujiunga na elimu ya
vyuo vya juu kimeongezeka kutoka wanafunzi 49,959 mwaka 2010/11 hadi
60,592 (asilimia 19).
Aidha, katika shule za sekondari umeongezeka kutoka wanafunzi
728,528 hadi 802,554 ikiwa (asilima 9.2) ukiwa ni uwiano wa wanafunzi wa
kike na wa kiume kuwa asilimia 44.8.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu,
alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa wakati akizumgumzia maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani leo.
Alisema vitendo vya ukatili kama ukeketaji vimepungua kutoka
asilimia 18 hadi asilimia 15 kwa mwaka 2010 wanatarajia kiwango hicho
kitapungua zaidi ifikapo mwaka 2015.
Mwalimu alisema wanawake wamewezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia elimu
ya ujasiriamali na mikopo yenye masharti nafuu kupitia benki ya
wanawake Tanzania hadi kufikia Juni 2012 ilitoa mikopo yenye thamani ya
Sh. bilioni 1.2 kwa wanawake 5,270 na wanaume1,157.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Uelewa wa masuala ya jinsia katika jamii,ongeza kasi’